Kulenga miundombinu ya kiraia ni uhalifu wa kivita - Balozi wa Iran katika UN
Balozi huyo wa Iran pia alionya kwamba iwapo Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama havitachukua hatua madhubuti, "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina haki yake, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ya kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kulinda mamlaka yake.
Muhtasari
Ujerumani yaripoti kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama
Mechi ya kuwania nafasi ya tatu: Jinsi Ufaransa ilivyofika hapa
Ufaransa ilifika nusu-fainali ya Kombe la Dunia kwa mbwembwe na nguvu kubwa, ikiwazidi nguvu wapinzani wake kupitia safu ya ushambuliaji yenye kasi na uwezo mkubwa, ikiongozwa na mabao nane ya Kylian Mbappe.
Hata hivyo, kikosi cha Didier Deschamps kilishindwa kuonyesha kiwango chake katika mchezo huo wa nusu-fainali dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Uhispania.
Wakiwa wamezidiwa na kuzuiwa na mtindo wa soka wa kumiliki mpira uliotumiwa na kocha wa Uhispania, Luis de la Fuente, walishindwa kurejesha udhibiti wa mchezo baada ya kufungwa bao la penalti na Mikel Oyarzabal katika kipindi cha kwanza.
Mechi ya mwisho ya Deschamps kama kocha wa Ufaransa
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, amezungumzia hisia za
kutotaka kucheza dhidi ya Uingereza lakini bado amesisitiza kwamba ni muhimu
kwa kikosi chake kufanya kila wawezavyo kujaribu kushinda mchezo huo:
"Nina wajibu katika mchezo huu," alisema
Deschamps.
"Huu si mchezo wa kirafiki. Ni mchezo wa kuwania nafasi
ya tatu. Wachezaji, benchi la ufundi na mimi tuna wajibu wa kufikia lengo hili
la mwisho.
"Haupewi uzito mkubwa kama fainali. Uingereza haitaki
kucheza mchezo huu na sisi pia hatutaki. Lakini ndiyo hivyo, tupo hapa.
"Lazima tuweke akili zetu kwenye lengo hilo la kushika
nafasi ya tatu na kulitimiza lengo hili la mwisho. Tuna wajibu huo tunapovaa
jezi hii.
"Najua akilini mwangu kuwa huu ni mchezo wangu wa
mwisho. Sitaki mtu yeyote alie. Mwisho umekaribia lakini maisha
yanaendelea."
Michuano ya Kombe la Dunia: Kinyang'anyiro cha tuzo la mfungaji bora
Mechi ya
timu ya tatu bora kwenye Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu inatarajiwa
kuandaliwa mwendo wa saa tano usiku wa Jumamosi Julai 18.
Ufaransa
ambayo ilikuwa katika fainali ya miaka minne iliyopita nchini Qatar itakuwa
inachuana na England ambayo ilikuwa na matumaini makubwa ya kunyakuwa taji hilo
ambalo walishinda mwisho miaka ya sitini.
Na huku
macho yote yakilenga vikosi hivyo kujuwa mbivu na mbichi watakuwa pia
wakiangazia ni nani mfungaji bora zaidi kwenye awamu ya mwaka huu.
Bado kuna
tuzo ambayo wachezaji wa pande zote mbili wataielekezea macho: tuzo ya mfungaji
bora (Golden Boot).
Nahodha wa
Ufaransa, Kylian Mbappe, amekuwa na michuano bora sana na kwa sasa anashikilia
nafasi ya pamoja na Lionel Messi kama wafungaji bora wa Kombe hili la Dunia,
wote wakiwa na mabao nane kufikia sasa.
Hata hivyo,
gwiji huyo wa Argentina kwa sasa ana faida kidogo kutokana na kutoa pasi nne za
mabao (assists) ikilinganishwa na tatu za Mbappe.
Mabao
yanayofungwa katika mechi za kuwania nafasi ya tatu huhesabiwa katika
kinyang'anyiro cha Kiatu cha Dhahabu; hivyo, Mbappe bado anaweza kumpiku
mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona—ingawa Messi naye atakuwa na fursa ya
kujibu mapigo katika mchezo wa fainali yenyewe.
Iwapo Mbappe
atafunga bao, au kutoa pasi mbili za mabao, angefuata nyayo za Salvatore
Schillaci wa Italia, ambaye alishinda Kiatu cha Dhahabu mwaka 1990 kwa kufunga
bao katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu dhidi ya… England.
Kombe la Dunia : Je, wachezaji wasiojulikana sana watapata nafasi ya kucheza?
Baada ya ratiba ngumu katika michuano hii ya Kombe la Dunia, kuna uwezekano makocha wote wawili wakatumia fursa hii kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wao nyota.
Hali hiyo inaweza kutoa fursa kwa wale ambao wamekuwa wakisubiri kucheza katika michuano hiyo.
Kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo, bado hajacheza hata dakika moja, lakini kwa kuwa mchezo huu hauna shinikizo kubwa, Tuchel anaweza kumpa kijana huyo mwenye kipaji nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia na kumpa mapumziko Declan Rice baada ya kuugua hivi karibuni.
Ollie Watkins naye anaweza kupata nafasi ya kucheza baada ya kutumika kwa dakika sita pekee hadi sasa—muda unaokaribiana na ule aliocheza Ivan Toney, ambaye aliingia akitokea benchi wakati England ikisaka bao la kusawazisha katika nusu fainali.
Kwa upande wa Ufaransa, bingwa wa mwaka 2018, N'Golo Kante, naye bado hajacheza, na akiwa na umri wa miaka 35, kuna uwezekano mkubwa hii ikawa fursa yake ya mwisho kucheza katika Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Rayan Cherki, amecheza kwa dakika 85 pekee katika michuano hiyo.
Je, Didier Deschamps anaweza kumpa nafasi ya kuanza mchezo?
Ujerumani yaripoti kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama
Waziri wa usalama wa Ndani wa Ujerumani ameonya kuhusu
kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama na kusema kuwa amepandisha kiwango cha
tahadhari ya usalama nchini humo hadi cha "juu zaidi"; hali ambayo
inaashiria kuwa shambulio linaweza kutokea wakati wowote.
Katika mahojiano na gazeti la *Welt am Sonntag*, Alexander
Dobrynt alisema kuwa kuna "ushahidi wa wazi" wa kuwepo kwa mipango ya
kushambulia watu, miundombinu, na taasisi za serikali nchini Ujerumani.
Aliongeza kuwa chanzo cha vitisho hivyo kiko nje ya
Ujerumani, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Serikali ya Kenya yakabiliana na wadukuzi wa Tovuti rasmi ya Rais
Serikali ya Kenya imesema kwamba imechukuwa hatua za dharura kupambana na udukuzi dhidi ya tovuti rasmi ya Rais William Ruto.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mchana wa Jumamosi Julai 18, Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa dijitali William Kabogo amesema kwamba wataalamu wamechukuwa hatua mwafaka za kudhibiti hali na kuwazuia wadukuzi kutekeleza hasara kubwa.
"Kwa wakati huu, hakuna ushahidi kwamba wenye kutekeleza uhalifu huo wamepata taarifa au data muhimu za serikali wala hakuna data ambayo imevuja wala kupotea. Mifumo ya serikali kwa pamoja na shughuli za kidijitali za serikali ziko salama na zinaendelea kama kawaida," alisema Waziri Kabogo.
Mamlaka ya kusimamia mawasiliano ya teknolojia {ICT AUthority} nchini Kenya imeripotiwa kushirikiana na taasisi husika za serikali kwa pamoja na kampuni za teknolojia zinazoshirkiana na serikali ya Kenya kufanya uchunguzi wa kina kupata tathmini ya kina kuhusu kiwango cha hasara ambacho huenda kimefanywa na wadukuzi hao.
Tovuti ya Rais wa Kenya: https://www.president.go.ke ilidukuliwa mapema Jumamosi hii huku wadukuzi wakiitaka serikali ya Kenya kuwalipa takriban shilingi milioni 41 za Kenya sawia na shilingi milioni 890 za Tanzania kabla ya kurejesha tovuti hiyo mikononi mwa serikali.
Hii si mara ya kwanza ya tovuti za serikali ya Kenya kudunguliwa na wahuni, mara ya mwisho, wadukuzi walilenga huduma muhimu za serikali kama vile E-citizen ambayo inatumika kwa malipo yote rasmi ya huduma za serikali.
Iran: Siasa ya "vita na mazungumzo kwa pamoja" imefikia mwisho
Mohsen
Rezaei mshauri wa kijeshi wa kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema
kuwa sera ya 'mazungumzo na vita kwa wakati mmoja' imefikia mwisho.
Alisema:
"Ikiwa Wamarekani wataendelea na mapigano katika siku mbili au tatu
zijazo, tutaingia katika awamu ya operesheni kamili ya kukera na
kuharibu."
Haya
yanajiri huku maeneo mengine ya kusini mwa Iran yakikumbwa na mashambulizi ya
anga ya Marekani jana usiku, usiku wa saba wa mapigano kati ya Iran na
Marekani. Iran ilitangaza kuwa Kuwait, Bahrain, Jordan na Saudi Arabia
zimeishambulia.
Katika
upande mwingine, ofisi ya rais wa Lebanon imetangaza kuwa Rais Joseph Aoun wa
nchi hiyo ameondoka leo Beirut na kuelekea Washington.
Anatarajiwa
kukutana na Donald Trump wakati wa safari hii na kujadili "kujiondoa kwa
Israeli kutoka kwa maeneo yanayokaliwa kwa sasa na Israeli."
Nchini Iran,
msemaji wa idara ya mahakama ametangaza kuwa kesi imewasilishwa dhidi ya Reza
Pahlavi.
Katika Picha: Rais wa Misri akikagua Gwaride la Jeshi la Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akikagua Gwaride rasmi la Mapokezi lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Julai Juni, 2026.
Maghala ya biashara ya mtandaoni Urusi yashambuliwa na Ukraine
Watu saba
wameuawa na wengine 49 kujeruhiwa baada ya ndege zisizo na rubani za Ukraine
kushambulia maghala mawili ya kuhifadhi bidhaa yanayomilikiwa na kampuni kubwa
zaidi ya Urusi ya biashara ya mtandaoni, Wildberries, kulingana na maafisa wa
Urusi.
Vifo vyote
na majeruhi 25 kati ya hao yalitokea katika ghala moja jijini Tambov, takriban
maili 295 (kilomita 475) kusini-mashariki mwa Moscow. Majeraha mengine 24
yalitokea katika ghala jingine la Wildberries huko Elektrostal, katika eneo la
Moscow.
Rais wa
Ukraine Volodymyr Zelensky alisema mashambulizi hayo yalilenga "vituo
muhimu vya usafirishaji na ugavi" ambavyo vilikuwa vikitumika
"kusambaza vipengele vilivyowekewa vikwazo kwa ajili ya utengenezaji wa
ndege zisizo na rubani na vifaa vya urambazaji".
Aliongeza
kuwa Ukraine pia ilishambulia maeneo lengwa katika Bahari ya Azov, Bahari
Nyeusi, na Crimea, eneo lililochukuliwa na Urusi.
Zelensky
alisema operesheni za Ukraine zilikuwa majibu dhidi ya "mashambulizi ya
Urusi kwenye miundombinu yetu ya kiraia na kwenye miji na jamii zetu".
Katika usiku wa kuamkia Jumatano, watu 14 waliuawa katika mashambulizi ya Urusi
kote Ukraine.
Wildberries
mara nyingi huchukuliwa kama kampuni ya Urusi inayolingana na Amazon. Kundi la
RWB lililoundwa kwa kuunganisha Wildberries na kampuni ya matangazo ya Russ,
lilikadiriwa kuwa na thamani ya takriban dola bilioni 12.6 (pauni bilioni 9.3)
na jarida la Forbes Russia.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Wildberries, Tatyana Kim, alisema ulikuwa "usiku wa
kutisha" kwa Urusi na kwa kampuni hiyo.
"Watu
saba waliokuwa wakifanya kazi zamu ya usiku walifariki papo hapo," gavana
wa eneo la Tambov, Evgeniy Pervyshov, aliandika kwenye Telegram, akiongeza kuwa
ndege zisizo na rubani 28 pia zilidunguliwa wakati zikikaribia eneo hilo.
Wakati huo
huo, gavana wa eneo la Moscow, Andrei Vorobyov, alisema baadhi ya watu
waliojeruhiwa katika mashambulizi kwenye ghala la Wildberries huko Elektrostal
walikuwa katika "hali mbaya".
Aliongeza
kuwa jumla ya ndege zisizo na rubani 48 zilidunguliwa katika eneo la Moscow
usiku huo, na kwamba ghala la mafuta la Urusi pia lilishambuliwa na ndege isiyo
na rubani iliyoanguka, tukio ambalo alilielezea kuwa lenye "madhara
makubwa zaidi".
"Wazima-moto,
huduma za dharura, na Wizara inayosimamia shughuli za udhibiti wa hali za dharura
wanaendelea kufanya kazi katika eneo la tukio," aliandika kwenye Telegram.
Hakuelezea
kwa kina kiwango cha uharibifu. Zelensky alithibitisha kivyake kuwa Ukraine
ilishambulia "kituo cha mafuta".
Tovuti rasmi
ya Rais William Ruto imedukuliwa, na ukurasa wake wa mwanzo umeharibiwa kwa
kuwekwa ujumbe unaomlenga Rais na kudai malipo ya fidia kwa njia ya Bitcoin.
Ukaguzi
uliofanywa na Kenyans.co.ke kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti hiyo
(president.go.ke) ulionyesha kuwa maudhui rasmi yalikuwa yameondolewa na badala
yake kuwekwa ujumbe wa dharau unaomlenga Mkuu wa Nchi.
Ukurasa huo
ulionyesha madai dhidi ya Ruto, anwani ya mkoba wa sarafu ya kidijitali
(cryptocurrency wallet) na agizo la malipo, huku wadukuzi hao wakitishia kutoa
taarifa ambazo hazikutajwa iwapo matakwa yao hayatatimizwa.
"Huu ni
ujumbe wa tatu kwako; kabla hatujavujisha kila kitu kukuhusu. Fanya malipo ya
Bitcoin 5 kwenye mkoba wa Bitcoin... Ikiwa unataka amani kabla ya saa kumi na
mbili jioni hii," ujumbe huo kwenye ukurasa ulioharibiwa ulisema.
Katika
taarifa fupi kwa chapisho hili siku ya Jumamosi, Julai 18, Ikulu ya Serikali
ilithibitisha kuwa ilikuwa inajua kuhusu udukuzi huo na kusema timu yake ya
TEHAMA ilikuwa ikishughulikia suala hilo.
Ikiwa Ikulu
ya Serikali itaheshimu mahitaji ya fidia, hesabu zetu zinaonyesha kuwa Hazina
italazimika kulipa Ksh 41,337,872.40 sawia na dola laki tatu za Marekani na
shilingi 838,605,411.25 za Tanzania. Hii inatokana na kiwango
cha ubadilishaji ambapo BTC 1 inafanya biashara kwa takriban Ksh 8,267,574.48.
Wadukuzi
walibadilisha bango la tovuti, wakionyesha ujumbe uliorejelea majina ya watu
watatu huku chapa rasmi ya Ikulu ikiendelea kuonekana nyuma.
Tukio hilo
limeibua wasiwasi kuhusu usalama wa miundombinu ya kidijitali ya serikali,
kwani bado haijulikani wazi ikiwa uvujaji huo uliwekwa kwenye ukurasa wa mbele
wa tovuti au ulienea kwenye mifumo yake ya nyuma.
Tukio la
hivi karibuni si mara ya kwanza tovuti za serikali ya Kenya kulengwa katika
shambulio la mtandaoni.
Mnamo mwezi Novemba
mwaka jana, tovuti kadhaa zinazomilikiwa na wizara na mashirika ya serikali,
ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu, Kazi, Mazingira, TEHAMA, Utalii, Mambo ya Ndani
na Ikulu, ziliathiriwa katika shambulio lililoratibiwa.
Washambuliaji
waliharibu tovuti zilizoathiriwa kwa kubadilisha maudhui rasmi na jumbe
zisizoidhinishwa na kufanya milango kadhaa ya serikali isipatikane.
Usumbufu huo
uliathiri huduma muhimu za mtandaoni zinazotegemewa na umma, huku baadhi ya
tovuti zikionyesha kauli mbiu kali na maudhui mengine yasiyoidhinishwa.
Hata hivyo,
Wizara ya Ulinzi na Hazina ya Kitaifa zilikuwa miongoni mwa taasisi
zilizoripotiwa kutoathiriwa na shambulio hilo la mtandaoni.
Shirika la ndege la Kuwait labadilisha ratiba ya safari zake nyingi za ndege
Shirika la
ndege la Kuwait limetangaza siku ya Jumamosi kuwa limebadilisha ratiba ya
safari nyingi za ndege kutokana na kusitishwa kwa muda kwa shughuli katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuwait kufuatia mashambulizi ya makombora ya
Iran na ndege zisizo na rubani.
Shirika hilo
la ndege hapo awali lilikuwa limesema kuwa mabadiliko ya ratiba ya safari ya
ndege hiyo yalitokana na kufungwa kwa anga ya Kuwait.
Kuwait
ilitangaza saa chache zilizopita kwamba imegundua na kunasa makombora ya
balistiki na ndege zisizo na rubani katika anga lake.
Kituo cha kuondoa chumvi kwenye maji chaharibiwa kabisa Iran
Abdul Hamid
Hamzapour, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka ya Mkoa wa
Hormozgan, amesema kuwa kutokana na shambulio la Marekani kwenye kituo cha
kusafisha maji cha Bunji magharibi mwa wilaya ya Jask, usambazaji wa maji ya
kunywa kwa wakazi wapatao 10,000 wa vijiji takriban 20 umetatizika kabisa, na
watu wa vijiji hivyo wamekabiliwa na uhaba wa maji.
Kwa mujibu
wa vyanzo vya habari, mashambulizi hayo yaliharibu kabisa kituo cha kusukuma
maji ghafi kutoka baharini, pamoja na transfoma ya umeme ya kiwanda cha
kusafisha chumvi cha Bunji, kilichokuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo
3,150 za maji mchana na usiku.
Argentina VS Uhispania: Ni kikosi kipi chenye safu kali ya ushambulizi kufunga mabao?
Lionel Messi anashiriki michuano ya tatu ya kombe la dunia huku Michuano ya 2026 yakiwa ya kwanza kwa Lamine Yamal kushiriki.
Zimesalia chini ya saa 36 kabla ya dunia kujuwa ikiwa Argentina watahifadhi taji lao au Uhispania itakuwa Bingwa wa Kombe la Dunia baada ya kushinda mwisho mwaka wa 2010 nchini Afrika Kusini.
Na kabla ya kutinga Fainali, timu hizi mbili zilikabiliwa na kibarua kigumu.
Kikosi cha Argentina kimejizolea jumla ya mabao 19 katika michuano ya mwaka huu, idadi kubwa ambayo wataalamu wanasema imetokana na uwezo wao mkubwa wa kushambulia goli na kufunga mabao.
Messi na wenzake wamefunga angalau mabao mawili katika kila moja ya mechi 13 ambazo wameshiriki, tangu kupoteza mechi yao dhidi ya Saudia Arabia 2-1 kwenye mechi yao ya kwanza katika michuano yaliyoandaliwa Qatar miaka minne iliyopita.
Na japo Uhispania imerusha makombora makali upande wa goli, safu yake ya ushambulizi imepenya na kufunga mabao sita pekee, huku wataalamu wakisema kwamba mchezo wao ni wa kadri.
Katika mechi zao, Uhispania imekuwa na nafasi kadha nzuri za kufunga mabao ila hazikutumika vyema.
Nao Argentina wamefunga bao moja tu ndani ya boxi ila mengine yote makali zaidi yamefungwa nje ya eneo hilo, huku wakifunga mabao matano kutoka mbali huku Uhispania ikikosa kufanya hivyo katika mechi zake.
Uhispania imefunga mabao sita chini ya idadi ya Argentina, ila wamefungwa mabao macheche hadi sasa – katika mechi ya robo fainali ambapo walifungwa bao moja na Ubelgiji, walishinda kwa mabao mawili dhidi ya Ubelgiji.
Argentina huenda wakijiona wamekosa kuwa na Bahati kwani wamefungwa mabao saba katika michuano ya mwaka huu, huku timu tatu pekee zikilinda goli lao dhidi ya mashambulizi na kutofungwa mabao mengi.
Lakini hata kama safu ya ulinzi ya Argentina imewahi kufanya vyema kuliko ilivyo kwa sasa, Uhispania imejitokeza kuwa katika kiwango bora cha mchezo.
Bila shaka, hata baada ya kucheza mechi zaidi ya 44, Uhispania bado ina kiwango kidogo cha tishio dhidi ya safu yake ya ulinzi kutokana na kufungwa hilo bao moja na Ubelgiji huku timu ya pili ambayo haikufungwa mabao mengi katika awamu ya makundi ikiwa Uruguay.
Balozi wa Iran katika UN: Kulenga miundombinu ya kiraia ni uhalifu wa kivita
Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa "amelaani vikali" mashambulizi ya Marekani dhidi ya miundombinu ya raia wa Iran katika barua kwa Baraza la Usalama.
Amir Saeed Irwani alisema kuwa mashambulizi ya mara kwa mara kwenye maeneo ya raia, hasa barabara na mitandao muhimu ya usafiri wa reli inachukuliwa kuwa "uhalifu wa kivita."
Balozi huyo wa Iran pia alionya kwamba iwapo Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama havitachukua hatua madhubuti, "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina haki yake, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ya kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kulinda mamlaka yake, ukamilifu wa mipaka yake, watu wake na maslahi yake muhimu."
Matukio yakuvutia katika michuano ya Kombe la Dunia 2026
“Patrice Lumumba” – shabiki wa DRC alisimama kama sanamu kushabikia ‘Leopards’
Mechi 104
zinatarajiwa kukamilika usiku wa Jumapili Julai 19 ambapo mbivu na mbichi
itajulikana wazi kuhusu ni nani Bingwa wa Kombe la Dunia katika Soka mwaka huu
wa 2026.
Na huku
Lamine Yamal wa Uhispania akijiandaa kukabiliana na mmoja wa wachezaji bora
duniani Lionel Messi, wengi watakumbuka mengi yaliyotokea kwenye maeneo ya
mashabiki kuketi, au hata nje ya uwanja lakini yalikuwa na uhusiano mkubwa na
kabumbu iliyokuwa ikisakatwa.
Haya hapa
matukio yaliyowavutia wengi hasa kwenye mitandao ya kijamii:
“Patrice Lumumba”, Shabiki wa Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo Michel Kuka Mbolandinga anayefahamika kama ‘Lumumba Vea
– au sanamu iliyohai,’ alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliokuwa uwanjani
na hata waliomtazama kwenye mitandao ya kijamii hasa wakati ambapo timu ya
taifa ya DRC ilipokuwa ikicheza mechi zao za makundi, awali kwenye michuano ya
mwaka huu.
Alipigwa
picha akiwa amesimama bila kusonga kwa muda wote ambao mechi zilikuwa
zikichezwa, akiwa ameinuwa mkono wake wa kulia na akiwa amevalia suti yenye
rangi za bendera ya taifa hilo.
Hatua hiyo
inafanana na sanamu ya kumuenzi aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Patrice
Lumumba ambayo ipo katika mji mkuu Kinshasa.
2: Ndugu mdogo wa Lamine Yamal avutia wengi
Mtangazaji
wa soka wa BBC Kelly Cates alimtaja kijana huyo mdogo kama mtoto mrembo
aliyewavutia wengi kwa uzuri wake. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu –
Keyne – ni kaka yake mdogo mshambulizi wa Uhispania Lamine Yamal – mwenye umri
wa miaka 19.
Na japo
ndugu yake mkubwa ni mchezaji maarufu wa Klabu ya Barcelona nchini Uhispania,
Keyne amejipatia umaarufu wa aina yake aliporekodiwa akijaribu kucheza mchezo
wa gofu, na kukerwa na kutokuwa na uwezo wa kuupiga mpira vyema miongoni mwa
mambo mengine.
Katika mechi
kati ya Ubelgiji na Uhispania, kijana huyo mdogo alipigwa picha ya video akiwa
amepakatwa huku akitabasamu kwa kuwa Uhispania ilikuwa imefuzu kuendelea mbele
baada ya kuicharaza Ubelgiji.
3. Haaland na
Bellingham wakijitokeza kama marafiki
Licha ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England kwa misimu kadhaa, Erling Haaland anaonekana hakuwa amepata umaarufu mkubwa nchini Marekani na Canada hadi sasa.
Hata hivyo, mambo yalibadilika kabisa msimu huu wa kiangazi baada ya mitandao ya kijamii kumuenzi mshambuliaji huyo wa Norway na Manchester City kupitia wimbi la 'meme' zilizotawala TikTok na Instagram, na kumjengea kile kilichoonekana kama ulimwengu wa kipekee mtandaoni.
Kulikuwa na mengi ya kuvutia mashabiki, huku Haaland akionekana pamoja na mwigizaji Channing Tatum. Baadaye akafunga mabao saba, akapata maelfu ya wafuasi wapya kwenye mitandao ya kijamii.
Erling
Haaland na Jude Bellingham wakikumbatiana baada ya England kuibuka na ushindi
dhidi ya Norway mjini Miami.
IShowSpeed
Mwanamitandao
maarufu IShowSpeed, anayejulikana kwa kuruka sarakasi za nyuma (backflips),
kubweka kwa utani na kuvaa jezi zilizogawanywa rangi mbili, atatumbuiza kwa
wimbo wake wa (World Cup) Champions katika sherehe ya kufunga mashindano kabla
ya fainali ya Jumapili.
Mshawishi
huyo wa mitandao ya kijamii ambaye pia hurusha matangazo yake moja kwa moja amekuwa
mmoja wa watu walionufaika zaidi na Kombe la Dunia la mwaka huu, akiongoza
vipindi vya kutazama mechi mubashara mtandaoni akiwa ndani ya viwanja wakati wa
michezo.
Kombe la Dunia: Marekani yatetea bango la wachezaji wa Argentina
Ikulu ya Marekani
imetetea timu ya taifa ya Argentina baada ya wachezaji wake kuonyesha bango
lililoandikwa "Las Malvinas son Argentinas" ("Visiwa vya
Falklands ni vya Argentina") kufuatia ushindi wao dhidi ya England katika
nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Hatua hiyo
imekosolewa na Uingereza huku Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) likitatarajiwa kuchukua
hatua za kinidhamu.
Andrew
Giuliani, mkuu wa kikosi kazi cha FIFA cha Ikulu ya Marekani, amesema wachezaji
hao walikuwa wakitumia haki yao ya uhuru wa kujieleza chini ya Marekebisho ya
Kwanza ya Katiba ya Marekani walipokuwa nchini humo, kwa mujibu wa BBC.
Bango hilo
linarejelea madai ya muda mrefu ya Argentina kuhusu visiwa vilivyoko kusini mwa
Bahari ya Atlantiki, vinavyojulikana kwa Kiingereza kama Falkland Islands na
kwa Kihispania kama Las Malvinas.
Serikali ya
Uingereza imekosoa kitendo hicho, huku Ikulu ikisisitiza kwamba Visiwa vya
Falklands "kwa hakika ni" vya Uingereza na kuunga mkono wito wa FIFA
kuchunguza iwapo bango hilo lilikiuka kanuni za shirikisho hilo zinazokataza
kauli za kisiasa wakati wa mechi.
Serikali ya
Visiwa vya Falklands pia imeeleza kusikitishwa kwake na kuitaka FIFA
kuichukulia hatua timu ya Argentina, ikisema haitaki kutumiwa kama "mpira
wa kisiasa".
Tumelenga kituo cha Marekani na madaraja kadhaa nchini Bahrain - Iran
Jeshi la Iran limetangaza kwamba katika awamu ya kumi na
tano ya Operesheni "Shine", limelenga "maeneo ya ndege pamoja na
matangi ya mafuta, katika kituo cha Sheikh Issa nchini Bahrain" kwa
kutumia ndege zisizo na rubani za kujilipua.
Taarifa hiyo pia ilidai kwamba madaraja kadhaa nchini
Bahrain yalilengwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani. Hata hivyo, si maafisa
wa Bahrain wala Marekani hakuna ambaye ametoa maoni juu ya kiwango cha
uharibifu au uwezekano wa kuwepo kwa majeruhi.
Mwanaharakati wa India aliyegoma kula kwa siku 20 apelekwa hospitalini kwa nguvu
Mwanaharakati
na msomi wa India Sonam Wangchuk, ambaye alikuwa kwenye mgomo wa kula kwa siku
20 zilizopita huko Delhi, ameondolewa kwa nguvu kutoka eneo lake la maandamano.
Mwanaume
huyo mwenye umri wa miaka 59 alikuwa akiandamana kuunga mkono harakati za
kejeli mtandaoni zinazoitwa Cockroach Janta Party (CJP) zinazotaka mageuzi ya
kielimu. Waandamanaji walikuwa wamepanga maandamano hadi bunge la India siku ya
Jumatatu.
Wangchuk
alikuwa amegoma kula chakula wakati wa kiangazi chenye joto kali, huku akila
chumvi na maji tu. Alikuwa amepunguza uzito zaidi ya kilo 9 na
alikuwa na maumivu makali.
Mwanzilishi
wa CJP Abhijeet Dipke sasa ameanza mfungo usiojulikana badala yake. Anasema
maandamano ya kuelekea bungeni yataendelea na amemtaka Waziri Mkuu Narendra
Modi ajiuzulu.
Dipke
aliambia BBC kwamba alikuwa ameenda nyumbani kwa rafiki yake asubuhi ili
kupumzika wakati polisi walipofika na kukataa kumruhusu aondoke.
Video kutoka
kwenye tovuti ya maandamano siku ya Jumamosi zilionyesha machafuko yakizuka
kabla tu ya saa 1:30 kwa saa za huko (02:00 GMT) wakati polisi kadhaa na
wanajeshi walipoingia ghafla kwenye jukwaa ambalo mwanaharakati huyo alikuwa
amelala. Waandamanaji waliojaribu kuwazuia walisukumwa mbali.
Walimfunika
kwa mapazia ya shuka kabla ya kumtoa jukwaani. Dakika chache baadaye, ambulensi
ilionekana ikiondoka kwa kasi.
Mke wa
mwanaharakati huyo Gitanjali Angmo baadaye alichapisha kwenye mtandao wa X
kwamba alikuwa "katika hospitali ya Safdarjung ambapo amelazwa".
Marekani yaishambulia Iran kwa usiku wa saba mfululizo
Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi kwa
usiku wa saba mfululizo dhidi ya Iran tangu Rais Donald Trump atangaze
makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda "yamefutiliwa mbali".
Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa X, Kamandi
Kuu ya Marekani (Centcom) iliandika kwamba vikosi vyake "vimeshambulia
maeneo ya uchunguzi, miundombinu ya vifaa vya kijeshi, maghala ya silaha yaliyopo chini ya
ardhi, na uwezo wa
kijeshi wa majini".
Jeshi la
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilisema meli mbili za mafuta
zililipuka katika Mlango-Bahari wa Hormuz wakati zikipita kwenye sehemu ya njia ya meli
iliyokuwa na mabomu ya ardhini. Taarifa hiyo ilipuuzwa na Hata hivyo, Centcom ilisema
kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Vikosi vya
kijeshi vya Jordan vilisema vilidungua makombora 10 ya Iran yaliyorushwa kwenye
anga yake usiku huo, ingawa hakukuwa na majeruhi wala uharibifu wowote.
Centcom
ilisema kuwa ilimaliza mashambulizi yake saa 21:30 kwa saa za Marekani
Mashariki (02:30 BST) baada ya kufanya mashambulizi hayo kwa muda wa saa
kadhaa.
Katika
taarifa yake, Centcom ilisema: "Vikosi vya Marekani vilitumia ndege za
kivita, ndege zisizo na rubani, na meli za kivita pamoja na vifaa vingine
katika operesheni hiyo."
Shirika la
habari la serikali ya Iran, Fars, lilisema meli mbili za mafuta
"zililipuka na kushika moto wakati zikipita kwenye njia iliyokuwa na
mabomu ya ardhini kusini mwa Mlango wa Hormuz". Baadaye, Centcom iliandika
kwenye X: "Kama madai mengi ya IRGC, hii si kweli."
Usafirishaji
wa meli katika Mlango muhimu wa Hormuz umesitishwa kwa kiasi kikubwa kutokana
na kuendelea kwa mashambulizi ya kulipizana kisasi kati ya vikosi vya Marekani
na Iran.
Facts Only
Iran's UN Ambassador, Amir Saeed Irwani, labeled attacks on civilian infrastructure as war crimes.
Iran's military advisor, Mohsen Rezaei, stated the policy of "simultaneous war and dialogue" has ended.
U.S. airstrikes targeted southern Iran and a desalination plant in Bunji, Jask district.
The Bunji desalination plant outage affected water supply for approximately 10,000 residents across 20 villages.
Ukraine used drones to attack two Wildberries warehouses in Tambov and Elektrostal; seven people were killed and 49 injured.
Germany's Interior Minister, Alexander Dobrynt, raised the national security alert level to the highest stage.
Hackers targeted Kenyan President William Ruto's official website, demanding 5 Bitcoin (approximately 41 million Kenyan Shillings).
Egypt's President Abdel Fattah El-Sisi inspected a military parade in Dar es Salaam, Tanzania, on July 18, 2026.
France and England are scheduled to play for third place in the 2026 World Cup on July 18.
Kylian Mbappe and Lionel Messi are tied with eight goals each in the World Cup tournament.
Argentina and Spain are scheduled to compete in the World Cup final.
Executive Summary
Global tensions are escalating across several fronts, characterized by kinetic warfare, cyber aggression, and heightened security alerts. In the Middle East, the conflict between Iran and the United States has intensified, with Iran signaling a shift toward "full offensive operations" following U.S. strikes on civilian infrastructure, including critical water desalination facilities. Simultaneously, Ukraine continues its campaign against Russian logistics, specifically targeting e-commerce warehouses to disrupt the supply of drone components, resulting in multiple casualties.
Cybersecurity vulnerabilities are evident in Kenya, where the presidency's official website was breached for ransom, reflecting a broader pattern of state-level digital instability. In Europe, Germany has moved to its highest security alert due to external threats. Amidst these geopolitical crises, the 2026 World Cup provides a stark contrast, transitioning from high-stakes athletic competition—highlighted by the rivalry between Argentina and Spain—to the logistical and emotional closure of the tournament for players and coaches.
Full Take
The strongest version of this narrative is a "world in friction," where the boundaries between civilian and military targets are blurring. From the destruction of Iranian water plants to the targeting of Russian commercial warehouses, the prevailing logic is that total mobilization requires the neutralization of all supporting infrastructure, regardless of its civilian nature.
The content is a fragmented news aggregate rather than a single authored argument. It juxtaposes the visceral brutality of war and state-level hacking with the celebratory atmosphere of a World Cup. This creates a jarring cognitive dissonance, reflecting a modern information diet where catastrophic geopolitical shifts and sports trivia occupy the same mental space. The narrative relies on a series of high-stakes declarations—specifically from Iranian officials—to create a sense of imminent escalation.
Patterns detected: none
The root cause is the erosion of the "civilian sanctuary" paradigm. We are seeing a shift where the " rear" of a nation (warehouses, water plants, websites) is now the "front line." The unstated assumption is that these escalations are inevitable results of state aggression, ignoring the possibility of strategic signaling or asymmetric desperation.
Human agency is diminished when critical survival infrastructure, like water, becomes a legitimate military target. The second-order consequence is the potential for total systemic collapse in localized areas, driving migration and instability that transcends the original conflict.
Bridge Questions:
1. If civilian infrastructure is targeted as a "response" to previous attacks, does the concept of a "war crime" still hold utility, or is it becoming a rhetorical tool rather than a legal restraint?
2. How does the simultaneous consumption of global sports and global warfare affect a population's psychological capacity to respond to crisis?
Counterstrike Scan:
A coordinated influence campaign would use this fragmented style to create a sense of "global chaos" to destabilize public confidence in international order. However, this text reads as a standard multi-topic news summary. It does not match the structural alignment of a targeted psychological operation.
Sentinel — Human
The text appears to be a composite of multiple, fact-heavy news segments, exhibiting the varied pacing and structural shifts typical of human aggregation rather than pure generative output.
