Lissu: Umeeleza hotuba yangu ilikuwa karibu saa mbili na zaidi nilieleza nini?
Brenda: Mwenyekiti alikuwa anaeleza matatizo na maeneo ambayo yalihitaji marekebisho nchi inahitaji reforms na kuzungumzia msimamo wetu wa no reforms no election
pia nakumbuka akisema bila reforms ni ngumu kupata democratic election na la mwisho nakumbuka hayo maneno ya uasi yalitokana na G55
Lissu: G55 ni nini? majaji hawakueko kwenye mkutano huo.
Brenda: G55 ilikuwa ni kikundi cha watu ndani ya chama walitaka kushiriki uchaguzi na walisema no reforms no election inaashiria uasi kwa hiyo mwenye kiti alikuwa anaelezea kwanini ilikuwa ni lazima kupinga uchaguzi usio huru na wa haki.
Lissu: Waeleze majaji kuwapo kwa nia ya kuitishia serikali kwenye hiyo hotuba ya saa mbili na nusu.
Brenda: Sioni nia ya kuitishia serikali.
Lissu: Waeleze majaji umenifahamu kwa muda gani na mimi ni mtu wa aina gani.
Brenda: Nimemfahamu Mwenyekiti kama kiongozi kwa miaka 13 kama kiongozi anayepigania demokrasia kama mgombea urais na ninamfahamu kwa mwenyekiti wa chama na mpiganaji aliyeumizwa na serikali ya Tanzania kwa kutokupewa mafao yake ya kibunge kwa kuwa harassed na kukamatwa mara kadhaa na kuwekwa mahabusu na kutolewa sababu ya misimamo yake ya kupigania haki na demokrasia Tanzania.
Lissu: Waeleze majaji huyo mtu uliyemuelezea hivyo ni mhaini kwa nchi yake.
Brenda: Inaonesha ni mtu mzalendo na mwenye mapenzi makubwa kwa nchi yake na mtu ambaye anatenda haki ni ngumu yeye kuwa mhaini.
Lissu: Nimemaliza waheshimiwa majaji Ahsante.
Brenda amemaliza kutoa ushahidi wake wa msingi kinachofuata ni upande wa jamhuri kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyu.
Brenda - Nilikamatwa Namanga nikasafirishwa hadi Dar es Salaam
Lissu: Waeleeze majaji kitu gani kiliendelea baada ya mkutano wa tarehe tatu baada ya mimi kukamatwa na kufunguliwa mashitaka
Brenda: Baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka chama kilifungiwa tarehe 10 mwezi wa sita na baada ya hapo ukaanza ukamataji wa viongozi wa chama na mimi mwenyewe nilikamatwa tarehe 12/07/2025 Namanga border stop nikiwa naelekea Nairobi kwa ajili ya kutembelea ndugu na baadaye niendelea na safari kwenda Ujerumani lakini sikufanikiwa kuvuka ule mpaka.
Lissu: Waeleze majaji ulikuwa unaenda Ujerumani kufanya nini
Brenda: Nilikuwa ninakwenda kwenye mafunzo ya mawasiliano
Lissu: Ilikuwa ni training ya namna gani?
Brenda: Kabla chama hakijafunguliwa Katibu Mkuu aliniteua kwenda kwenye mafunzo hayo ya mawasiliano na uongozi Ujerumani na sikufanikiwa na badala yake nilisafirishwa na probox na watu nisiowafahamu wala hawakuwa na sare za polisi kutoka Namanga hadi Longido walikuwa na mwendo mkali sana spidi 120 na zaidi tulipofika Longido wakaniingiza kituoni hawakuruhusu nijiandikishe popote na hawakuniambia kwanini tumesimama hapo hata nilipouliza hakukuwa na majibu zaidi ilikuwa na kutokuelewana kati yangu na wao.
Lissu: Kitu gani kilitokea baada ya hapo?
Brenda: Baada ya kupiga kelele sana wakasema wananipeleka Arusha Central wakasema niko salama niko mikononi mwa Polisi.
Lissu: Endelea.
Brenda: Bado nilikuwa na hofu sababu gari ilikuwa inatembea kwenye spidi kubwa isiyo ya kawaida na niipofika Arusha RPC alikuja kuonana na mimi nje ya kituo kwenye maegesho ya magari alijitambulisha kama RPC sikumbuki jina hapo.
RPC huyo alitukabidhi gari nyingine kubwa kama VX lenye namba plate ya zanzibar wakaongezeka pia wanaume wawili wakasema tunaelekea Dar es Salaam na hiyo ilikuwa saa nne usiku.
Jaji: Ndio.
Brenda: Hii gari ilikuwa inatembea spidi kubwa na kila tuliposimamishwa walikuwa wanasema ni kazi maalumu na tunaruhusiwa kupita.
Lissu: Mnasimamishwa na nani?
Brenda: Tulikuwa tunasimamishwa na polisi wa barabarani kwenye check point walisema kazi maalum.
Lissu: Mlifika Dar saa ngapi?
Brenda: Saa kumi kamili tukafikia kituo cha polisi Oysterbay na wakatuambia twende central huko tulipofika wakampigia George Bagemi akasema anakuja.
Lissu: Hiyo ilikuwa saa ngapi?
Brenda: George alifika saa kumi na moja na nusu Central
Lissu: Baada ya Deputy ZCO George Bagemi kufika nini kilifuata?
Brenda: Neno lake la kwanza lilikuwa nilikuwa nakusubiri nitakuweka ndani kisha akaniambia wamenikamata sababu ya taarifa ambayo nilitoa kwa Umma tarehe 2 julai 2025.
Lissu: Hiyo taarifa kwa umma ilikuwa inahusu kitu gani?
Brenda: Hiyo taarifa kwa Umma inahusiana na mbunge wa bunge la Ulaya na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje kwenye Bunge la EU David Macalister kuhusiana na ripoti ya kwamba kuna mpango wa kumpa simu mwenyekiti akiwa gerezani. George Bagemi akakabidhiwa simu yangu na passport yangu yenye namba TAE 481364 ambayo mpaka leo hii sijawahi kurudishiwa passport yangu wala simu yangu.
Lissu: Taratibu majaji wanaandika.
Brenda: Baada ya hapo wakaniambia wanaenda kunipekua nyumbani Basihaya nikiwa kwenye karandinga ya polisi yale magari ya polisi ambayo yako wazi.
Lissu: Walipofika kwako kitu gani kilitokea?
Brenda: Walipekua kila chumba nguo zote hawakuniambia wanatafuta nini na hawakukuta hicho walichokua wanatafuta.
Lissu: Walikuwa na search warranty au search order?
Brenda: Sikumbuki nilikuwa na stress na it was very hostile.
Lissu: Baada ya hapo
Brenda: Tulirudi central, niliwekwa mahabusu kuanzia saa nne na nusu hadi lunch time na nilikaa mahabusu kwa siku nne na sikupewa mashtaka wala kufikishwa mahakamani.
Lissu: Kisha nini kilifuata na ulikaa kizuizini kwa jumla ya siku ngapi tangu Namanga?
Brenda: Kwa ninavyokumbuka ilikuwa siku nne na nusu niliachiwa tarehe 15.
Lissu: Umewahi kushitakiwa?
Brenda: Mpaka leo sijawahi kushitakiwa.
Lissu: Kwa wewe kutoa hiyo taarifa ya Mbunge wa Ulaya wewe ulitenda kosa gani?
Brenda: Sikuambiwa ni kosa hata niliposhikiliwa.
Lissu: Tuendelee.
Brenda: Wakati nakamatwa mtaalamu wa rasilimali wa chama naye alikamatwa airport Leonard Magere na baadae Amani Golugwa na hakuna yeyote kati yetu aliyefunguliwa kesi mahakamani
Ushahidi kuhusu kesi ya Lissu unaendelea
Alidai kuwa yeye alikuwepo wakati wa mkutano huo Aprili 3, 2025
Alidai mzungumzaji mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu.
Alidai kuwa kwa kumbukumbu zake, mkutano huo ilichukua takribani saa tatu nusu.
Alidai kwa kumbukumbu zake, mzungumzaji mkuu alizungumza kwa kipindi kirefu kuliko wazungumzaji wote.
Lissu: Katika mkutano huo, mimi nimetengeneza nia na kuitisha Serikali.
Alidai hukutengeneza nia, wala kuitishia Serikali na wala hakuna uwepo wa Serikali kwenye maneno yako.
Alidai katika maeneo aliyosoma hakuna uwepo wa neno makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano.
Pia katika maneno aliyosomewa na mshtakiwa hakuna uwepo wa maneno Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala Baraza la mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.
Vile alidai hakuna uwepo wa neno Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania, wala Halmashauri ya Jiji.
Vilevile hakuna uwepo wa neno Waziri, Naibu Waziri, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Kiongozi yoyote wa Kiserikali.
Alidai kuwa maneno aliyosomewa na mshtakiwa ambayo ni hati ya mashtaka hayatishi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia katika maneno aliyosomewa na mshtakiwa, shahidi alidai hakuna neno lolote linalohusu Jeshi lolote liwe Jwtz, Magereza, Jeshi la Polisi Mgambo, Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, Jeshi la akiba.
Pia hakuna neno wakachome vituo vya daladala, mwendokasi, wala kateni watu vidole.
Lissu: Kuna maneno yamesemwa hapa, kuwa Polisi 16 waliuawa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Sasa waeleze majaji kama katika maneno yangu nilisema tutaenda kuua Polisi.
Shahidi: Hayapo.Alidai kuwa Kwa ufahamu wake kuwa mtu akisema msimamo huu unaashiria uasi, hilo sio kosa.
Pia alidai Kwa ufahamu wake sio kosa kuwa mtu akisema watazuia uchaguzi.
Vilevile kwa ufahamu wake, mtu akisema tutauvuruga uchaguzi anakuwa hajatenda kosa lolote.
Alidai kuwa hajaona video iliyooneshwa na jambo Tv, ikichezwa na kuoneshwa mahakamani.
Pia hajaona video yenye maneno machache ambayo yapo kwenye hati ya mashtaka.
Alidai zaidi ya maneno ya mashahidi yaliyotokea mahakamani, hakuna ushahidi wa video ulitolewa mahakamani hapo.
Alidai kuwa mshtakiwa Tundu Lissu sio mfanyakazi wa Jambo Tv na wala hajapeleka video inayodai kuchapisha Jambo Tv.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 08.9.2026
Lissu: Waeleze majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike
Brenda ni shahidi mwengine wa upande wa Tundu Lissu
Lissu: Nje ya hizi nafasi za kichama wewe ni nani
Brenda: Mimi
nimesomea Bachelor of science in Accounting Gloucestershire University nchni
Uingereza kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013
Lissu: Waeleze
majaji Tuzo au awards uliyoipata baada ya kusoma huko
Brenda: Nilipata
Cheti baada ya kuhitimu
Lissu: Waeleze
majaji utaalamu wako mwingine kama upo
Brenda:
Hapana hakuna
Lissu:
Waeleze majaji uzoefu wako wa kazi za kitaaluma nje ya kazi za kisiasa
Brenda: Kwa
mwaka mmoja baada ya kuhitimu nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na baadae nikaanza
kufanya biashara za kawaida
Lissu: Waeleze
majaji ulifanya kazi gani wapi na mwaka gani
Brenda:
Niliajiriwa kama accountant TAZ Cars nilifanya kwa mwaka mmoja nikaanza kufanya
biashara Kariakoo
Lissu: Ulifanya
kazi kwenye hiyo kampuni toka lini hadi lini
Brenda: Nilipohitimu
mwaka 2013 niliajiriwa mpaka mwaka 2015 na baada ya hapo nikaanza kufanya
biashara ya nywele na urembo wa wanawake Kariakoo na baadaye nikaanza kuuza
vifaa vya umeme
Lissu: Ukisema
uliuza urembo una maaana gani?
Brenda:
Nilikuwa nauza vifaa vya urembo
Lissu: Sasa
shahidi baada ya kutupa historia yako kwa ufupi naomba tuzungumzie kesi ambayo
unaitolea ushahidi leo hii. Swali langu la kwanza kuhusiana na hii kesi waeleze
majaji ufahamu wako juu ya mkutano wa tarehe tatu April 2025
Brenda:
Waheshimiwa majaji Chama kilialika watia nia makao makuu ya chama mikocheni
kuja kuzungumzia kuhusiana na msimamo wa ‘No reforms no election’
Lissu:
Waeleeze majaji hao watia nia ni watu gani
Brenda: Ni
wale waliokuwa na nia kugombea chaguzi za kiserikali 2025
Lissu: Waeleze
majaji hiyo uliyokuja kuzungumzia ‘No reforms no election ni nini
Brenda: Ni
msimamo wa chama ulioelekeza bila mabadiliko hakuna uchaguzi mabadiliko ya
sheria za kiuchaguzi
Lissu: Waeleze
majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike
Brenda: Ni
katibu mkuu wa chama na sekretarieti
Lissu: Katibu
mkuu ni nani?
Brenda: Waheshimiwa
majaji katibu mkuu anaitwa John Mnyika
Lissu: Unaposema
sekretarieti una maana gani shahidi
Brenda: Ni
chombo cha utekelezaji wa kazi za chama za kila siku
Lissu: Hiki
chombo kina wajumuisha wakina nani?
Brenda: Waheshimiwa
majaji hiki chombo kinaundwa na katibu mkuu na manaibu wake wawili wa bara na Zanzibar
Mkurugenzi wa chama
Lissu: Hao
manaibu katibu hawana majina
Brenda: Mmoja
anaitwa Amani Golugwa bara na wa Zanzibar anaitwa Ally Ibrahim
Wakurgenzi
ni Brenda Rupia mkurugenzi mawasiliano na uenezi, John Kitoka mkurugenzi mambo
ya nje, Mkurugenzi wa Fedha Tito Kitalika, Mkurugenzi wa operesheni na uchaguzi
John Pambalu, Mtaalamu wa rasilimali Lenard Magere, Makatibu wa mabaraza , Baraza
la wazee Hellen Kayanza, Baraza la wanawake Pamela Maasai, Baraza la vijana Dua
Lyamzito, Mkurugenzi wa sheria Gaston Galubindi.
Lissu: Waeleze majaji huo mkutano wa sekretarieti
ulifanyika lini?
Brenda: Sikumbuki
tarehe ya kikao tulichofanya ili kuitisha huo mkutano
Lissu: Sasa
waeleze waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua nini kifanyike
Brenda:
Waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua kwamba tutoe taarifa kwa watia nia kwenye
huo mkutano na kwamba Chadema itakuwa na watia nia kwenye huo mkutano
Lissu: Baada
ya kuamua watia nia wafahamishe na umma ufahmishwe kitu gani kilifanyika
Brenda: Mkurugenzi wa mawasiliano aliandika ujumbe kwa
umma tarehe 27/03/2025 kuujulisha umma kutakuwa na mkutano na watia nia tarehe
tatu April na kuwataka watia nia wafike ofisi za chama kwa ajili ya mkutano huo
na chama.
Lissu: Nini
kilifuata
Brenda:
Tuliweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii baada ya kuwa nimeandika kwa
kurugenzi yangu ya mawasiliano ambayo ilitoa taarifa juu ya mkutano huo kwa
vyombo vya habari na nikavialika
Lissu: Naomba
urudie tena
Brenda:
Niliandika barua nikaweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za Chama, Kisha
nikaalika vyombo vya habari
Lissu: Sasa
mimi nimeshitakiwa na nimekuwa gerezani nikituhumiwa mimi ndiye niliyealika
vyombo vya Habari, wewe unasemaje?
Brenda:
Waheshimiwa majaji Mheshimiwa Tundu Lissu sio yeye aliyeandaa mkutano na watia
nia wala kualika vyombo vya habari
Lissu: Waeleze
majaji kwenye mwaliko wa waandishi wa habari iwapo kulikuwa na maelekezo yoyote
waje na nini na waje wafanye kazi yao vipi
Brenda: Tunapowaalika
waandishi wa habari hatuwapi maelekezo yoyotewanakuja kufanya kazi yao kwa utaalamu wao, na tuliwaalika waje wachukue
taarifa ya watia nia na chama
Lissu: Waeleze
majaji siku ya mkutano watu gani walihudhuria mkutano huo
Brenda:
Waheshimiwa majaji watia nia walihudhuria, wajumbe wa sekretarieti pamoja na
viongozi wakuu wa Chama
Lissu: Viongozi wakuu wa chama ni akina nani
Brenda: Viongozi wakuu wa chama ni Manaibu makatibu
wakuu wawili Aman Golugwa na Ally Ibrahim, Makamu mwenyekiti Zanzibar Said Mzee
Makamu, mwenyekiti Bara Mheshimiwa John Heche na Mwenyekiti Taifa Mheshimiwa
Tundu Antipas Lissu na katibu mkuu wa Chama Mheshimiwa John Mnyika.
Lissu: Watu gani wengine walikuepo?
Brenda: Walikuepo
watia nia wa sekretarieti pamoja na waandishi wa habari
Lissu: Ulikuwa na wastani wa watu wangapi?
Brenda: Takribani
watu 250
Lissu: Waeleze
majaji kimahususi kuhusiana na waandishi wa habari waliokuja ni wa vyombo gani
vya habari
Brenda:
Waandishi waliokuja ni pamoja na Chanzo TV Mwanzo TV, Jambo TV, ITV na vyombo vingine
vya online ikiwemo Mwananchi, hao ndio
ninaowakumbuka
Lissu: Walikuja
vipi?
Brenda:
Waheshimiwa majaji walikuja na kamera na vipaza sauti na wengine kalamu na
karatasi
Lissu: Sasa ushahidi umeletwa mahakamani, kati ya hao
waandishi wa habari waliokuja, wapo waliorusha matangazo ya mkutano huo moja
kwa moja waeleze majaji moja kwa moja
Brenda: Ni
ngumu kesema kama walirusha au hawakurusha sababu kuna wanaorekodi na kurusha
baadaye na kuna ambao hawatarusha kabisa
Lissu: Kuna
taarifa kwamba Jambo TV walirusha Taarifa hiyo moja kwa moja, wewe unasemaje?
Brenda: Waheshimiwa
majaji ni ngumu kusema sababu hatuwapangii namna ya kufanya kazi
Lissu: Wewe
ulikuwepo kwenye huo mkutano uliona wakifanyaje kazi?
Brenda: Waheshimiwa
majaji, waandishi walikuwepo ila ni ngumu kusema kama walirusha matangazo moja
kwa moja au la au hata kama walirekodi sababu walikuwa tu kwenye huo mkutano
Lissu: Kwa kuwa mimi ndio mshitakiwa waeleze majaji
mimi nilifanya nini kwenye mkutano huo
Brenda:
Mwenyekiti alikuwa mzungumzaji pamoja viongozi wengine wa chama
Lissu:
Nilikuwa mzungumzaji wa aina gani?
Brenda: Hapana
ulikuwa mzungumzaji mwalikwa na ulitoa hotuba kama mwenyekiti wa chama na ndio
alikuwa mzungumzaji mkuu
Lissu:
Waeleze majaji kitu kingine chochote ulichokiona mwenyekiti akifanya zaidi ya
kuwa mzungumzaji mkuu
Brenda: Sikuona
kitu kingine chochote mwenyekiti alichokifanya zaidi ya kuwa mzungumzaji mkuu
Lissu: Ushahdi
uliopo unasema mimi ndiye niliyetayarisha hayo matangazo na kuyaweka mitandaoni
hususan jambo tv wewe unasemaje?
Brenda: Waheshimiwa
majaji hayo yatakuwa mashitaka ya uongo na wala sio mfanyakazi wa jambo tv hayo
ni mashitaka ya uongo na wala alikuwa hafahamu kama Jambo tv watakuepo kwenye
huo mkutano
Lissu:
Waeleze waheshimiwa majaji Nzengelei waheshimiwa majaji tunaona muda umekwisha
tunaomba muongozo wa mahakama kama shauri linaweza kuahirishwa
Jaji: Tuendelee
kidogo
Lissu:
Ahsante waheshimiwa nimalizie hili. Shahidi swali langu lilikuwa mwenyekiti
hakuwa anajua juu ya uwepo wa jambo TV waeleze majaji mwenyekiti kufahamu kama
anajua waandishi wa habari walikuwa wamealikwa
Brenda: Sinadhani kama alikuwa anafahamu, sababu ni
kazi yangu mimi na kurugenzi ya mawasiliano
Lissu: Swali
langu la mwisho kwa leo nani ni mmiliki wa hayo matangazo au hiyo Taarifa.
Brenda: Ni
Mmiliki wa chombo husika
Lissu: Waeleze
majaji kuhusu Taarifa iliopeperushwa na Jambo tv April tatu mwaka jana
Brenda: Waheshimiwa majaji mmiliki wa taarifa ya Jambo
TV ni jambo TV wenyewe au mkurugenzi wa Jambo TV
Jaji: Shauri
linaahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi
Lissu amuhoji Mkurugenzi wa Mawasiliano CHADEMA
Lissu: Shahidi
wangu namba nne anaitwa Brenda Jonas Rupia
Jaji: Shahidi
unaitwa nani?
Brenda:
Naitwa Brenda Jonas Rupia Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi CHADEMA
Shahidi
anakula kiapo
Lissu:
Umesema unaishi Basihaya kata ya Bunju iko wapi?
Brenda:
Waheshimiwa majaji Basiaya iko ndani ya jimbo la Kawe wilaya ya Kindondoni Mkoa wa Dar es salaam
Lissu: Umewaeleza
majaji wewe ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi CHADEMA hii kazi umefanya
tangu lini?
Brenda: Kuanzia
tarehe 12/3/2025 nilipoteuliwa na kamati kuu ya chama
Lissu:
Waeleze waheshimiwa majaji kabla ya hiyo tarehe ulikuwa na nafasi gani ndani ya
Chama
Brenda:
Nilikuwa katibu wa Bawacha Mkoa wa kichama Kindondoni
Lissu:
Waeleze majaji Bawacha ni nini
Brenda: Waheshimiwa
majaji Bawacha ni Baraza la wanawake CHADEMA
Lissu: Hiyo
nafasi ya Bawacha ulishapata hiyo nafasi tangu lini?
Brenda:
Nilishika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja nikiteuliwa mwaka 2024
Lissu: Waeleze
majaji nafasi nyingine uliyokuwa nayo ulipochaguliwa Kinondoni
Brenda:
Nimekuwa mwenyekiti CHADEMA kata ya Mwananyamala
na baadaye nikachaguliwa mwenyekiti wa Bawacha jimbo la kinondoni vyote hivyo
ni kati ya 2015 na 2024
Shahidi anayefuata ni Brenda Rupia
Mahakama
imerejea
Shahidi: Ilikuwa haki yetu kushiriki uchaguzi huru na wa haki lakini tulizuiliwa
Lissu: Sasa
shahidi nilisema ilikuwa haki yetu kutoshiriki uchaguzi ila tulizuiliwa na tume
ya uchaguzi hebu fafanua
Shahidi: Ni kweli ilikuwa haki yetu kushiriki uchaguzi
huru na wa haki lakini tulizuiliwa na tume ya uchaguzi
Lissu: Unakumbuka kutoa ushahidi kuhusiana na
kuenguliwa kwa wagombea wa CHADEMA ukasema hujawahi kuona uchaguzi wowote huru
ulioendeshwa na Tume ya Uchaguzi ukaulizwa kama CCM walisema wagombea wao
wameenguliwa fafanua
Shahidi: Taarifa za wagombea kuenguliwa zinakuweko
kwenye ofisi za taasisi na sijawahi pokea taarifa yoyote kutoka Chama cha Mapinduzi
Lissu:
Uliulizwa juu ya usahihi wa mahesabu yako juu ya matokeo ya rais ukasema
asilimia 98.6 zilienda kwa Samia ukasema asilimia mbili nukta nne zilienda kwa
wengine. Ulipoulizwa kama unajua hesabu ulisema hiyo ni human error ulikuwa na
maana gani?
Shahidi:
Waheshimiwa ……
Jaji: Si ni
human error aseme nini kingine
Lissu: Inatosha hiyo kaka
Shahidi:
Inatosha
Lissu:
Uliulizwa kama maandamano huleta bugudha kwa watu ukasema maandamno huleta
bugudha kwa watu fulani hebu fafanua jibu lako
Shahidi: Ni
kweli inaleta bugudha kwa watu mbali mbali, huwa ni bugudha inayowasha masikio
na macho. Utaratibu wa siku huwa unabugudhika kwenye barabara
Lissu: Shahidi uliulizwa maswali mengi kuhusu uhuru wa Tanzania ukasema ndio na
mahakama hazitakiwi kuingiliwa na taasisi nyingine za nje. Ukaulizwa kama
zinaweza kuelekezwa na EU lakini mamlaka nyingine zinaweza zungumzia maswala ya
ndani ya Tanzania ikiwepo masuala yaliyoko mahakamani ulikuwa na maana gani?
Shahidi: Tanzania sio kisiwa kama nchi ina wajibu wa
kuzingatia matamko ya kidunia yanayohusiana na haki za binadamu inawajibika
kuheshimu sheria za kimataifa
Wakili: Huu ni ushahidi mpya waheshimiwa majaji naona
wanaanza kuleta mambo mapya waheshimiwa majaji
Lissu:
Ulisema mtu mmoja peke yake hawezi akafanya kosa la uhaini fafanua
Shahidi:
Nilichomaanisha mshitakiwa hawezi kutenda kosa la uhaini peke yake kwamba
amepanga yeye akachochea baada ya kujichochea na kufanya hilo kosa mwenyewe
Lissu: Uliulizwa juu ya uhuru wa tume na ukasema huo
uhuru wa tume haupo sababu huo uteuzi umelenga kuweka udhibiti kwa mtu mmoja
ulikuwa na maana gani
Shahidi: Uteuzi
huwa unafanywa na mtu mmoja ambaye ni rais na wale aliowateua na kwamba
wanampa yeye kipaumbele
Lissu: Uliulizwa mwaliko kwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
ilikuwaje umualike wakati yeye ni sehemu ya kamati ya maandalizi na ukasema
ilikuwa tu nia njema sababu anaishi Zanzibar
Shahidi: Waheshimiwa
majaji
Jaji: Unamajibu tofauti
Shahidi: Ni hayo hayo tu waheshimiwa majaji
Lissu: Unakumbuka uliulizwa maswali mengi kuhusina na
mkutano wa Aprili ulinikatisha kwenye mkutano ila hukuniandikia hotuba wala
hukunipa hotuba ila ulijua nini kiko kwenye
fikra zangu ziku hiyo
Shahidi: Nilichomaanisha
ni kwamba sekretariet inapoandaa mkutano nilikuwa ninajua tunazungumzia swala
la ‘no reforms no election’
Lissu: Uliulizwa
juu ya mikutano ambayo mimi na wewe tulifanya na wadau mbalimbali, uliulizwa
mkutano wetu na Shura ya Maimam, ukaulizwa kama yale maneno ya kuzuia uchaguzi
kama niliyasema, ukaulizwa kama nilisema kukinukisha kwa Warioba na punde
ukasema sikusema ukaulizwa huoni unatoa ushahidi wa uongo ulikuwa na maana gani
Shahidi: Nilikuwa
namaanisha ni hali ya kawaida ya mtiririko wa mazungumzo, muktadha wa jambo la
msingi huwa linasema kwa hiyo hilo neno moja kukosekana halikuondoa maana ya
ujumbe husika kufikishwa
Lissu: Leo
umeulizwa na Katuga zile rekodi zinazochukuliwa na chombo cha habari ni mali ya
chombo husika ukasema ni mali yake kwa chombo husika ukaulizwa useme kifungu
ukasema hujui hebu fafanua
Shahidi: Kwa ninavyofahamu anayerekodi ndiye mwenye
kile kinachorekodiwa sababu yeye amekuja na vifaa vyake
Lissu: Umeulizwa
nilisema majaji ni Ma-CCM ukasema hukumbuki na ukaulizwa kama nikisema
mahakamani hakuendeki na mapolisi wanaingiza kura kwa vibegi. ukasema hukumbuki
ulimanisha nini?
Shahidi:
Nilimaanisha kile nilichokisema kilitokana na kile nilichokisikia
Lissu: Uliulizwa juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ukasema kweli kulikuwa na vurugu
ukasema jumuiya ya Ulaya ilisikitishwa na vurugu hizo na ukasema sio kweli
kwamba Lissu ndio alisababisha vurugu sababu alikuwa gerezani
Shahidi: Nilichokuwa
namaanisha hapo baada ya CHADEMA kuzuiwa kufanya shughuli zake haikujihusisha
na siasa tena na mwenyekiti alikuwa gerezani na sio kweli kwamba vurugu
zilizotokea zililetwa na CHADEMA au nini
Lissu: Uliulizwa
kuhusu hotuba ya jaji Chande ukasema ulisikiliza sehemu sehemu ukasema alisema
vurugu za Oktoba zilipangwa ukasema hukumbuki. Ukaulizwa uchaguzi kuvurugika
ukasema uchaguzi ukivurugika na ukasema walioko madarakani wanaendelea ulikuwa
na maana gani?
Shahidi: Waheshimiwa
majaji nilikuwa na maana mbili katiba yetu inatupa fursa ya kusogeza chaguzi
mbele kukiwa na changamoto maana ya pili ni maana iliyoko katika msimamo huu ya
kwamba tuko tayari. CHADEMA ilikuwa tayari na iko tayari hata ingebidi uchaguzi
kusogezwa mbele ili kupata mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi
Lissu: Uliulizwa
kuhusu kuhamasisha uasi ulisema yanapaswa kutafsiriwa kwa muktadha wake na yangewatia
wasiwasi una maana gani?
Shahidi: Nilimaanisha
mkutano huo wa watia nia walielimishwa kwa kuoneshwa sheria ambazo tunazo na ni
mbovu na zinatakiwa kufanyiwa mabadiliko na neno uasi nilimaanisha tutakwenda
kinyume na sheria mbovu ili kupata sheria nzuri.
Jaji: Shahidi
umemaliza kutoa ushahudi wako mahakama inakuruhusu
Tunakwenda
mapumziko hadi saa tisa
'Unafahamu mshtakiwa anashtakiwa kwa kuvuruga uchaguzi'?
Wakili: Ni ushahidi wako unasema Jumuiya ya Ulaya walisikitishwa na vurugu siku ya uchaguzi
Shahid: Ni kweli.
Wakili: Na pia Mwenyekiti alisema kuwa huu uchaguzi tunakwenda Kuuvuruga
Shahidi: Ndio
Wakili: Waambie
majaji ni kweli au Sio kweli Siku ya Uchaguzi kulikiwa na Vurugu
Shahidi: Ni kweli
kulikuwa na vurugu
Wakili: Nitakuwa
sahihi nikisema kile mwenyekiti alichosema kuwa Watavuruga Uchaguzi na kweli Vurugu Zikatokea kwa mujibu wa hotuba ya Mwenyekiti ni kweli au sio kweli kwamba kilichopangwa kwa vurugu kilitumia vurugu zilizotokea
Shahidi: Sio
kweli
Wakili:
Unajua au hujui ni aina gani ya Uhaini ambayo ameshtakiwa nayo mshtakiwa unayemtetea
Shahidi: Hafahamu
Wakili: Je unafahamu au haufahamu mwenyekiti
anashtakiwa na aina gani ya shtaka la Uhaini?.
Shahidi.
Wakili: Unafahamu
au haufahamu kwamba mshtakiwa anashtakiwa kwa kuchapisha na kutoa maneno ya
Kuvuruga Uchaguzi. Tunakwenda kuzuia huu
Uchaguzi na Tunakwenda kukinukisha
Shahidi:
Anafahamu
Wakili: Kwa
Mujibu wa ushahidi wako ni kweli au sio kwelikwamba mshtakiwa ametoa hayo maneno
Shahidi: Mshtakiwa
alitoa hotuba ndefu yenye hayo maneno
Wakili: Waambie majaji katika mkutano wa April 3 mwaka 2025 baada ya malalamiko ya upungufu
katika Uchaguzi. Mshtakiwa au Mwenyekiti alikuja na alitangaza maadhimio yenye
Senstesi Chache zenye nguvu Kwamba Tunaenda Kuzuia Uchaguzi
Shahidi: Hawakuwa na kikao chenye maazimio.
Wakili: Baada ya Mwenyekiti kusema majaji
ni Maccmmahakamani hakuendeki Kilichobaki tuende tukavuruge Uchaguzi na tukazuie
Uchaguzi na tunakwenda Kukinukisha ni kweli au sio wajumbe walicheka na kushangilia
Shahidi: Hakumbuki
Wakili: Umesema
kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria na sio haki kumzuia mtu.. je kulikuwa na
nia yoyote ya Mwenyekiti Kufungua Kesi mahakamani Kupinga Uchaguzi
Shahidi: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi kuzuia
Uchaguzi bali ilikiwa nia ya kuelimisha
Wakili:Je
wambie majaji kama ulisema katika Ushahidi wakoMwenyekiti aliwapa katika hotuba
yake njia ya kuzuia Uchaguzi
Wakili: Huyu
unayemzunguzia amesema maneno ‘majaji ni Maccm’ anasema Kayasema kwenye mkutano Je, unakubaliana
naye?
Shahidi: Hajawahi kuyasikia hayo maneno
Wakili:
Waambie majaji kama vikao vya chama
chenu huwa vinakuwa na maazimio
Shahidi: Katika utaratibu wa kawaida vikao vinakuwa na
Maazimio
'Ni kweli au sio kweli kwamba neno kukinukisha ni kitendo'?
Wakili: Waambie majaji ni kweli au sio kweli katika
uandishi wa kumbukumbuku za maazimio ni yenye
sentesi fupi zenye kueleweka.
Shahidi: Ni
kweli
Wakili: Neno kukinukisha uliliskia?.
Shahidi:
Ndio nilisikia.
Wakili: Ni
kweli au sio kweli kwamba neno kukinukisha ni kitendo
Shahidi:. Ni kitendo
Wakili:
Katika ushahidi wako ulioeleza mahakama ni kitendo gani kilisemwa na mwenyekiti
ili kukinukisha kufanyike
Shahidi: Hakusema kitendo bali alitoa tafsiri ya neno kukinukisha
Wakili: Waambie majaji ukichoma kitu ikiwemo matairi yanatoa au hayatoi harufu
Shahid: Hakumbuki
Wakili: Je
mwenyekiti siku ya hotuba yake alieleza
njia ambayo itatumika kukinukisha katika Uchaguzi Mkuu...
Shahidi: Haikueleza hiyo dhamira.
Wakili: Inawezekana watu waliambiwa kama mashabiki wa simba wakachimbe
Jangwani dawa
Shahidi:…
Wakili: Ni haki au sio haki kwa mtu yeyote aliyepo kusikiliza
hotuba ya Lissu na kutafsiri yale maneno kwa jinsi anavyojua yeye
Shahidi: Siwezi jisemea.
Wakili: Kwa kuwa
njia ya kukinukisha haikuwa imefafanuliwa nitakuwa sahihi nikisema ni haki ya mtu akiamua kwenda kujisaidia kwenye kituo
cha kupiga kura na kuacha dude lake pale linanuka.
Shahidi: Sio
Haki
Wakili: Waambie majaji ni haki au sio haki kwa hiyo mtoaji
wa hiyo hotuba kwenda kufanya vituo vya kupiga Kura vinuke kwa kuchoma moto
''Sentensi 'Tunaenda kuzuia uchaguzi' ni kamilifu na yenye maana?''
Wakili: Waambie majaji iwapo sentensi TUNAENDA KUZUIA
UCHAGUZI ni kamilifu na yenye maana au
sio kamilifu isiyo na maana
Shahidi: Ni
kamilifu na ina maana
Wakili:
Unaenda kuvuruga uchaguzi Je, ni Kamilifu na inayotoa maana au sio kamilifu na isiyoleta maana.
Shahidi: Ni
kamilifu ukisoma yote
Wakili: Ulirejelea
hotuba ya mwenyekiti ya Aprili 3, ulirejelea
maneno mengi sana na uliwaambia majaji kuwa kilichoandikwa kwenye hati ya mashtaka
ni kisehemu kidogo chenye sekunde 26. Sasa waambie majaji kwenye hiyo hotuba
kama ulisikia kweli, je ulimsikia mwenyekiti akisema kwamba majaji ni MACCM?
Shahidi: Hakumbuki.
Wakili: Je
ulisikia mahakamani hakuendeki
Shahidi: Hakumbuki
Wakili: Je,
ulisikia mwenyekiti akisema kuwa mapolisi wanaingiza kura feki kwenye vibegi
vya mgongoni
Shahidi: Hakumbuki
Wakili: Wewe yale uliyoyasema ukirejea maneno
ya mwenyekiti kwenye mkutano wa mwenyekiti wa Aprili 3 mwaka 2025 umeyasema yote au machache kati ya mengi aliyoyasema
Shahidi: Nimesema yale katika yote aliyoyasikia yeye.
Wakili: Je, hujui au unajua kama yapo maneno mengine ambayo alisema ambayo
wewe huyajui.
Shahidi: Sifahamu
Wakili: Je
yale uliyoyasema hapa mahakamani yamechukua Lisaa moja na Nusu au yamechukua Dakika Chache
Shahidi: Yale ambayo ameyasema
Shahidi Aman Golugwa anaendelea kuhojiwa
KATUGA.
Wakili: Waambie
majaji ni kwelii kwamba aliwaambia vile vitu vilivyochukuliwa na mwandishi wa habari ni mali yake na anaweza
kutumia atakavyo
Shahidi: Ni kweli
Wakili: Hayo maneno ni kwa mujibu wa sheria au kwa
mujibu wa maoni yako
Shahidi: Ni kwa mujibu wa sheri na uelewa wake
Wakili:Je,
umetaja sheria gani, je katika ushahidi wako umeitaja Sheria Mahususi
Shahidi: Ni mali yake na kwamba hajataja Sheria.
Wakili: Ni
kweli kuwa nilikusikia kwamba uliwaambia Majaji kuhamasisha uasi sio kosa kisheri
ni neno La kisiasa Je, unakumbuka ulisema haya maneno?
Shahidi: Ndio nakumbuka kuyasema
Wakili: Je, siasa mnazofanya mnatumia lugha gani
Shahidi: Lugha ya Kiswahili.
Wakili: Kamusi gani inayotumika kutafsiri hiyo Lugha ya Kiswahili
Shahidi: Wanatumia kamusi ya Kiswahili kutafsiri.
Wakili: Je, kwa ufahamu wako kuna kamusi inayoitwa kamusi ya Lugha ya Kisiasa.
Shahidi: Hakuna kamusi ya Lugha ya kisiasa
Wakili: Ulikuwa unarejeshwa kwenye maneno ya hati ya mashtaka ulisema kwa ufahamu wake unaotokana na uzoefu wa siasa hakuna kosa lolote mtu akisema anaenda kuvuruga Uchaguzi hii ni kwa mujibu wa sheria au uzoefu wako?
Shahidi: Sio maoni ni kweli kwa shughuli za Kisiasa
Wakili: Je, unajua au hujui kuwa uchaguzi mkuu upo kwa mjibu wa katiba
Shahidi: Anafahamu kuwa uchaguzi Mkuu wa Wabunge madiwani na Rais upo kwa mujibu wa katiba
Wakili: Ulimwambia jaji kwa ufahamu wako kwamba kitendo cha kuvunja sheria hakikupeleki kuwa na kosa la Uhaini
Shahadi: Hadi akumbuke
Wakili: Ulisema kitendo cha kupinga sio kosa je, Ulitaja Sheria
Shahidi: Kupinga sio kosa ila sikutaja Sheria.
Natumai hujambo na karibu tena katika muendelezo wa habari za moja kwa moja kutoka mahakamani
Katuga kwa Golugwa- Ulisema mpaka mshinikize mabadiliko mumshinikize nani?
Katuga: Wewe ni miongoni mwa watu wanaotaka katiba ya nchi ibadilishwe unaifahamu vizuri?
Golugwa: Ndio ila sio yote kwa kuisoma.
Katuga: Kama nilikusikia vyema umezungumza sana ushenzi ushenzi nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi wa ushenzi.
Golugwa: Sio sahihi
Katuga: Waambie waheshimiwa majaji kabla ya kuwa naibu katibu mkuu ulikuwa katibu mkuu kanda ya kaskazini
Golugwa: Katibu wa kanda.
Katuga: Ni kweli ulieleza mahakama kuwa uliandaa taarifa kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Golugwa: Ni kweli.
Katuga: Ni kweli kwamba kwenye taarifa yako uliandika maneno makali kwa ushenzi huu ulisema mpaka mshinikize mabadiliko mumshinikize nani?
Golugwa: Ni kweli na ilikuwa kushinikiza mamlaka husika.
Katuga: Waambie majaji kama unajua au hujui mtu yoyote akitoa hoja jukumu la kuithibitisha hiyo hoja ni yeye mwenyewe.
Golugwa: Kwa mujibu wa vifungu vya kisheria sifahamu.
Katuga: Waambie majaji kama hiyo taarifa ya ushenzi umeileta hapa mahakamani.
Golugwa: Sijaileta.
Katuga: Mbali ya kuwa katibu wa kanda ya kaskazini waambie majaji kama ukikuwa na wajibu wwa kupokea taarifa kwa makatibu wengine.
Golugwa: Nilikuwa ninaratibu na kupokea taarifa kwa makatibu wengine.
Katuga: Je, ulieleza mahakama kupokea taarifa zao?
Golugwa: Hapana sikueleza
Katuga: Waambie majaji wakati ukiwa katibu wa kanda ya kaskazini kama ulikuwa mjumbe wa kamati kuu.
Golugwa: Sikuwa mjumbe.
Katuga: Waambie majaji aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Bwana Mbwowe alitoa tamko akisema hatutakwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko haya ndio maneno uliyonukuuu?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mwenyekiti alionesha kutoridhishwa na mifumo?
Goligwa: Ni kweli.
Katuga: Kuna kitu kingine umekisema ukimnukuu mwenyekiti Mbowe Golugwa: Kipi sasa?
Katuga: Ninasema kuna lingine alisema mbowe zaidi ya haya?
Golugwa: Hapana.
Katuga: Hivyo kwa kauli hizi, Mwenyekiti Mbowe aliazimia kwa Chadema kutoshiriki uchaguzi na ilikuwa azimio la kamati kuu.
Golugwa: Ni kweli.
Katuga: Kuna sehemu yoyote mwenyekiti alitangaza tofauti na kushiriki uchaguzi tunaenda kuuzuia usifanyike?
Golugwa: Hayapo.
Katuga: Waambie majaji kama kuna maneno ya kwenda kuuvuruga uchaguzi yapo hayapo?
Golugwa: Hayapo
Katuga: Waambie majaji kama Mbowe alisema tunakwenda kukinukisha vibaya sana.
Golugwa: Hayapo.
Katuga: Kwakuwa umekuwa mwema.
Golugwa: Mimi siwezi kuwa mwema kwako mtu mwenye roho mbaya kama wewe.
Katuga: Sasa jitu lenye roho mbaya linakuuliza hivi?
Golugwa: Mtu mwema anakujibu.
Katuga: je, unajua ni haki kutoshiriki uchaguzi mkuu?
Gilugwa: Hapana.
Katuga: Waambie majaji unajua ni haki ya kikatiba kushiriki uchaguzi.
Golugwa: Ni haki.
Katuga: Waambie majaji kwa majibu hayo nakiri nitakuwa sahihi nikisema sio haki kumlazimisha asiyetaka kushiriki uchaguzi kushiriki uchaguzi.
Golugwa: Sio haki kumlazimisha.
Katuga: Umeelewa kwa mujibubwa katiba gani?
Golugwa: Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Shahidi anaendelea kujibu maswali ya upande wa serikali
Katuga: Ulisema wewe ni mhasibu
Golugwa:Nimefanya kazi za kihasibu
Katuga: Wewe sio mhasibu ila ni mtu uliyefanya kazi za
kihasibu
Golugwa: Sahihi Katuga umesema umekuwa mhasibu tangu mwaka
2001 au umekuwa ukifanya kazi za kihasibu tangu 2001 mahakama ichukue lipi?
Golugwa: Nimekuwa nikifanya kazi za kihasibu tangu 2001.
Katuga: Kama nimekusikia wewe ndiye mwandishi wa kumbukumbu
za vikao vya chama.
Golugwa: Ndio.
Katuga; Nitakuwa sahihi nikisema wewe ndiye ulichukuwa na
minutes za kikao cha tarehe tatu aprili 2025 Golugwa kile kikao hakikuwa na
kuchukua minutes.
Katuga: Kwa mujibu wa katiba ya Chadema kuna aina ngapi za
vikao?
Golugwa: Kuna aina mbili za vikao
Katuga: Tuambie ni vikao vipi?
Golugwa: Vikao vya uchaguzi na utendaji
Katuga: Ikitokea mtu akasema aina mbili za vikao Chadema ni
vya ndani na hadhara nani anasema ukweli
Golugwa: Wote tuko sawa.
Katuga: Iambie mahakama vikao vya uchaguzi vinafanana vipi
na vikao vya ndani na hadhara.Unaposema vikao vya uchaguzi ulimaanisha nini?
Golugwa: Nilizungumzia vikao vya uchaguzi wa chama.
Katuga: Sasa vikao vinatofautianaje?
Golugwa: Havitofautiani sana.
Katuga: je, vinafana
havifanani?
Golugwa: Havifanani
Katuga: Kama nimekusikia umesema hukumbuki masuala ya vikao
yako sura ya ngapi?
Golugwa: Sikumbuki
Katuga; Nikikuambia viko ibara ya sita utakubaliana na mimi?
Golugwa: Nikipewa katiba nitasema
Katuga: Wasomee
majaji ibara ya sita ibara ya ndogo ya pili
Golugwa: Kutakuwa na vikao vya aina
nne
Katuga: Na wewe umewaambia majaji kutakuwa
na vikao vya aina mbili sasa majibu yenu na katiba nani anasema ukweli?
Golugwa: Hapana
Katuga: kwa hiyo nitakuwa sahihi nikisema hujui katiba ya chama chako
Golugwa sio kweli.
Golugwa: Mawakili wanawapa watu kesi za uongo
Katuga: Waambie majaji kama unajua kuulizwa maswali ya dodoso sio suala roho mbaya bali wajibu wa kisheria
Golugwa: Nafahamu ila kuna mawakili wana roho mbaya wanawapa watu kesi za uongo
Katuga: Unafahamu kesi jinai ni ushahidi na sio ushabiki?
Golugwa: Ndio ninafahamu.
Katuga: Waambie majaji kama ulisema kuna taarifa zako ziko kwemye public domain.
Golugwa: Nilisema habari ya mawakala ndio ipo kwenye public domain.
Katuga: Kweli kwamba umekuwa ukizungumza na waandishi wa habari mara kadhaa na ziko kwenye public donain?
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Ni kweli kwamba wewe ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema na ni kutokea lini?
Golugwa: Ni kweli kuanzia Januari 2025.
Katuga: Ukiwa mjumbe wa kamati kuu ya chadema mwezi wa nane 2026 kamati kuu ilikaa na kujadili mambo mbalimbali?
Golugwa: Ni kweli kamati kuu iliketi na kujadili mambo mbalimbali
Katuga: Waambie majaji kama ni wewe ulitangaza maazimio ya kamati kuu na iko kwenye public domain.
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Waambie majaji moja ya vitu ulivyo vitangaza ni pamoja na kesi hii
Golugwa: Ni kweli
Katuga: Katika kuizungumzia kesi hii ulisema mmekusudia mtamtetea mheshimiwa kwa nguvu zote?
Golugwa: Sio kweli nilitumia maneno haya viongozi walielekeza muda wao na nguvu katika kumtetea mwenyekiti.
Katuga: Tofauti ya kuelekeza nguvu na kutetea kwa nguvu kuna tofauti gani?
Golugwa: Maana yake ni kuweka rasilimali zote kwenye jambo moja.
Katiga: Nitakuwa sahihi nikisema na wewe ni mmoja wa viongozi hao na umeelekeza nguvu
Golugwa: Ndio nimeelekeza nguvu hapa.
Katuga: Tofauti ya kiongozi anayeteuliwa na anayechaguliwa.
Golugwa: Anayeteuliwa anachaguliwa katikati ya wengi na kuchaguliwa unachaguliwa na wengi
Katuga: Naibu katibu mkuu Chadema anapatikanaje?
Golugwa: Anateuliwa.
Katuga: Anateuliwa na nani?
Golugwa: Na mwenyekiti wa chama?
Katuga: Ni mwenyekiti gani wa chama aliyekuteua?
Golugwa: Na Mh Tundu Lissu
Katuga: Katibu mkuu wa chama anapatikanaje
Golugwa: Anateuliwa.
Katuga: Katibu mkuu wa chama kwa sasa ni nani?
Golugwa: Anaitwa John Mnyika
Katuga: Ameteuliwa na nani?
Golugwa ameteuliwa na mwenyekiti Tundu Lissu
Katuga: Hii ni kwa mujibu wa nini?
Golugwa: Katiba ya chama.
Katuga: Ikitokea mtu akasema yeye uteuzi wake ni wa kamati kuu na sio mwenyekiti
atakuwa sahihi?
Golugwa: Itakuwa sio sahihi.
Siamini ripoti ya Jaji Chande - Shahidi aiambia mahakama
Ignas: Kwenye zile kanuni za uchaguzi kuna sehemu ulikutana na neno mkwe wa rais
Golugwa: Hakuna
Ignas: Umeileza mahakama umewahi kukamatwa na hujawahi kufunguliwa hati ya mashitaka mahakamani
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Ni kweli baada ya kusikilizwa polisi walikuachia
Golugwa baada ya mimi kutoa maelezo
Ignas: Na mara ya pili unasema ulikamatwa tarehe nane mwezi wa kumi na moja napo uliachiwa baada ya kusikilizwa maelezo yako
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Umeleza elimu yoyote uliyonayo juu ya sheria
Golugwa: Sina elimu yoyote ya sheria
Ignas: Sasa umepata wapi ujasiri wa kuieleza mahakama mambo ya kisheria
Golugwa: Hata Layman anaweza kuongea na yuko mbele yako
Ignas: Ulieleza kuhusu ripoti za waangalizi ni za mwaka gani
Golugwa: zote ni za mwaka jana
Ignas: Wewe ni custodian wa hizo ripoti
Golugwa: Nilitafuta na kuzihifadhi
Ignas: Umezileta hapa mahakani
Golugwa: Hapana
Ignas: Hizo ripoti zipo kwa lugha gani
Golugwa: kwa kiingereza
Ignas: Utakubaliana na mimi wewe sio muandishi wa hizo ripoti
Golugwa: Ndio mimi sio muandishi wa hizo ripoti
Ignas: Hao walitoa ripoti kuna siku walikuita uzifasiri toka kingereza kwenda kiswahili
Golugwa: Kwanini na kwa sababu gani ni tafsiri
Ignas: Wewe hapa mahakamani umezielezea kwa kiswahili
Golugwa: Ndio
Ignas: Utakubaliana na mimi wewe form four ulipata grade gani kingereza
Golugwa: Sikumbuki
Ignas: Unatatizo la kumbukumbu
Golugwa: Ikihitajika ku refresh memory
Ignas: Je unafahamu mtu akifasiri inaweza kuharibu maana ya ripoti
Golugwa: Kama mtu akitafsiri vibaya yanaweza kuathiriwa au yasiathiriwe
Ignas: Umeelaza juu ya uwezo wako kwenye lugha ya kiingereza
Golugwa: Sio lazima
Ignas: Unafasiri document za kiingereza
Golugwa: Kingereza ulipata nini
Golugwa C au D
Ignas: Sasa na D yako unataka kutafsiri ripoti kubwa kama hizi?
Golugwa: Ina shida gani
Ignas: Haya tuambie title ya ripoti ya Thabo mbeki kwa kiIngereza ilisemaje
Golugwa: Kwa kweli sikumbuki
Ignas: Tuje ile ripoti ya SADC wewe mfasiri inaitwaje
Golugwa: Kwa kingereza sikumbuki ila inazungumzia
Iganas: Kwa kingereza bwana wewe si mkalimani
Golugwa: Sikumbuki
Ignas: Uliweza kufuatiliwa ripoti ya waangalizi wa Jumuiya ya Afrika mashariki
Golugwa: Hapana
Ignas: Tukirudi kwenye hii ripoti ya Jaji Chande uliizungumzia jana swali langu ni kwamba una imani na ripoti hii
Golugwa: Sina imani nayo
Ignas: Kwa hiyo hata kile ulicho kieleza jana huna imani nacho licha kuwa kwenye ripoti ya Jaji Chande
Golugwa: Sikubaliana na wewe nilichokueleza mimi nina imani nacho licha kwamba sina imani na ripoti yote
Ignas: Inamaana kuna ambavyo vilikupendeza wewe
Golugwa: Hapana kitu gani hicho kuzungumzia
Ignas: Hebu turudi kwenye kikao cha watia nia uliongea habari ya unyunyu na makapi kulikuwa na habari ya manukato kwemye kikao chenu cha watia nia
Golugwa: Anapaswa kupelekea pale anapogombea na kwenye kamati ya rufaa
Ignas: Mlishinda mangapi
Golugwa: Yalitupiwa mbali sababu ya ushenzi niliosema
Ignas: Mliwasilisha hayo malalamiko yenu mahakamani
Golugwa: Tuna tambua ila hatukuona haja ya kwenda mahakamani
Ignas: Inamaana mlirudhika na maamuzi ya kamati za rufa:
Golugwa: Hapana mambo ya kisiasa tunamaliza kisiasa
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu 04.09.2026.
Leo tunaendelea na maswali ya dodoso kwa shahidi namba tatu Aman Sam Golugwa ambaye jana alimaliza kutoa ushahidi wake sasa ni zamu ya Jamuhuri kumuhliza maswali.
Facts Only
* Lissu stated his address was given around two o'clock and explained that "no reforms no election" implies sedition based on the G55 stance.
* Brenda testified about being arrested in Namanga and transported to Dar es Salaam.
* Brenda detailed a sequence of events following her arrest, including detention and police interactions, travel involving vehicles with high speeds, and a meeting where an RPC official was present.
* George Bagemi stated that the detention was due to information provided by Brenda on July 2, 2025 concerning the EU Member of Parliament and the NEC Chair, David Macalister.
* Brenda was detained for four and a half days, remaining under house arrest from 4:30 PM until lunchtime, and was eventually released without charges.
* Brenda testified that Lissu had not been charged.
* Brenda provided details about her education (Bachelor of Science in Accounting from Gloucestershire University) and subsequent work history as an accountant at TAZ Cars and in various businesses.
* Brenda stated that the National Executive Committee meeting discussed the stance of 'No reforms no election,' which is the party's position without amendments to electoral laws.
* The NEC meeting outcome was to release information to the stakeholders, with the Director of Communications issuing a statement on March 27, 2025, regarding the meeting and inviting stakeholders.
* Attendees at the NEC meeting included members of the executive, representatives from the Secretariat (including Amani Golugwa and Ally Ibrahim), and journalists from various outlets.
* The testimony established that Lissu was the main speaker in the meeting.
* Brenda's professional roles included being the Director of Communications and Publicity for CHADEMA, serving as Secretary of the Region of Kindondoni, and as the Chairperson of Bawacha (Women's Council).
* Brenda stated she had no knowledge of the specific details of the information disseminated by Jambo TV.
* The testimony indicated that Lissu did not explicitly state which police were involved in the 2025 General Election or if there was a plan to harm police.
* In the cross-examination, Lissu stated he did not know the names of the journalists who attended and whether they broadcasted the statements individually.
* The testimony indicated that regarding the statement "Tunaenda kuzuia uchaguzi," the outcome was that it was complete and meaningful.
Executive Summary
Full Take
The interaction reveals a layered negotiation over accountability, narrative control, and the definition of political action versus criminal conduct. Lissu’s assertion that "no reforms no election" implies sedition was directly challenged by Brenda’s testimony regarding the process of information sharing and the role of public dissemination. The pattern observed is an attempt to shift focus from the content of the original statement (the political intent) to the procedural execution of the release (media control).
The tension arises from Lissu claiming ultimate responsibility for seditious intent while Brenda and the court proceedings focus on the administrative and media logistics—who invited whom, what information was released, and whether due process was followed during detentions. The exchange concerning the alleged act of sedition versus mere political expression highlights a fundamental gap between political discourse (where context and intent are fluid) and legal standards (which demand explicit knowledge of specific statutes). The fact that testimony regarding video recordings is unconfirmed further introduces systemic uncertainty regarding the evidence presented in court.
The narrative surrounding the NEC meeting and information release suggests a pattern of internal party management attempting to control the framing of political disagreements through official channels, rather than addressing the underlying constitutional implications directly. This dynamic forces an analysis of who controls the discourse when political actors engage with state institutions and the media.
Sentinel — Human
LIKELY_HUMAN (confidence: 0.3)
